Jumapili 4 Oktoba 2026 - 15:00
Waislamu wa Texas Wajitokeza kwa Ushiriki Madhubuti katika Uchaguzi wa Marekani

Hawza/ Kutokana na kubadilika misikiti ya Texas kuwa vituo vya ushiriki wa kiraia wa wananchi, idadi ya Waislamu wanaojitolea kushiriki katika uchaguzi wa Marekani, kwa lengo la kufikia haki zao, imeongezeka kwa kiwango kikubwa.

Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Waislamu wa Texas wamesema katika mahojiano kwamba wakati huu wanataka sauti yao iwafikie wanasiasa wa jimbo hilo. Ushiriki umeongezeka kutoka wapiga kura 88 katika awamu iliyopita hadi zaidi ya wapiga kura 700 katika awamu ya sasa, huku waliojisajili wakitarajia kusajili takriban wapiga kura wengine 100.

Saher Salood, Mkurugenzi wa Utafiti wa Taasisi ya Sera na Uelewano wa Kijamii, alisema kuwa; kuongezeka ushiriki wa kiraia miongoni mwa Waislamu wa Marekani hakukumshangaza, kwa kuzingatia maadili anayoyafahamu miongoni mwa Waislamu wa Marekani. Salood alisema: “Jambo hili linaeleweka kabisa kwangu.”

Utafiti wa taasisi ya Salood unaonesha kwamba mwaka 2016, asilimia 60 ya Waislamu wa Marekani waliokuwa na sifa za kupiga kura walikuwa wamejisajili kupiga kura. Kufikia mwaka 2024, kiwango hicho kiliongezeka hadi asilimia 85. Salood alisema mwenendo huu umeambatana na kuongezeka kwa kauli za chuki dhidi ya Uislamu.

Aliongeza: “Ushiriki huu unafanyika wakati ambao, kuanzia mwaka 2022 hadi 2025, hisia za chuki dhidi ya Uislamu miongoni mwa umma zimeongezeka kwa kiwango kikubwa.”

Nchini Texas, mzunguko huu wa uchaguzi unatofautiana kwa namna ya pekee. Saher Salood alisisitiza: “Sijawahi kuona aina hii ya hotuba tunazoziona katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi.”

Chanzo: NBC News

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha